Mafundi wa Kikosi cha KMKM wakishusha Boti aina ya Faiba iliyomalizika kutengenezwa katika Kiwanda cha Kutengenezea Boti aina ya FAIBA kinachomilikiwa na KMKM Ngara Kibweni Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji, Mudrik Ramadhan Soraga (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kiwanda cha Kutengenezea Boti aina ya FAIBA kinachomilikiwa na KMKM Ngara Kibweni Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Zanzibar,Kushoto kwake ni Mkuu wa KMKM Komodoo Azana Hassan Msingiri.
Mkuu wa KMKM Komodoo Azana Hassan Msingiri akitoa hotuba wakati akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Boti aina ya Faiba kinachomilikiwa na KMKM Ngara Kibweni Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji, Mudrik Ramadhan Soraga akitoa hotuba ya ufunguzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Boti aina ya Faiba kinachomilikiwa na KMKM Ngara Kibweni Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Zanzibar. (PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR).