KVZ,Mlandege FC zatoshana nguvu ufunguzi Kombe la Mapinduzi 2023

NA DIRAMAKINI

KVZ na Mlandege FC za Zanzibar zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1katika mchezo wa michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Ni kupitia mtanange wa ufunguzi Januari Mosi, 2023 ambao ulipigwa dimba la
Amaan jijini Zanzibar.

Katika mtanage huo,mchezaji Mukrim Juma Madai wa KVZ alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.

Katika mchezo huo miamba hao walionekana kushambuliana kwa vipindi hadi mapumziko walikuwa hawajafungana.

Mlandege ilionekana kuwazidi wapinzani wao kwa kila idara huku wachezaji wake wakileta mashambulizi ya mara kwa mara , lakini umakini mkubwa ulioneshwa na mlinda mlango wa KVZ, Ibrahim Abdalla Rashid ambaye aliokoa mashuti yaliyokuwa yakilengwa langoni mwake.

Aidha, Mlandege ambayo inafundishwa na kocha Abdalla Mohammed Juma 'Bares', wachezaji wake walitengeneza mashambulizi manne ya nguvu ambayo mawili yalikoswa na Abdulnassir Asaa ambalo moja liligonga posi dakika ya 38 na moja likachezwa na mlinda mlango wa KVZ.
Mashambulizi mengine mawili ambayo Mlandege watajutia ni yale ya Yussuf Suleiman dakika ya 15 na Masoud Khamis Haji dakika ya 24 ambayo yaliokolewa na mlinda mlango wa KVZ.

KVZ wao katika kipindi cha kwanza walitengeneza nafasi moja dakika ya tatu kupitia mchezaji wake, Rahim Shomari ambalo alilipaisha juu.

Kipindi cha pili kilianza na mashambulizi yakaendelea ambapo dakika ya 46 Mohammed Said Mohammed 'Mesi' akaifugia timu yake bao la kuongoza ambalo dakika mbili baadae wakasawazishiwa baada ya mlinzi wa KVZ, Mukrim Juma Madai kujifunga wakati wa kuokoa mpira uliopigwa na Abdulnassir Asaa Gamal na kuingia moja kwa moja wavuni.

Januari 2, 2023 kutakuwa na michezo miwili ambapo saa 10:15 Namungo FC kutoka Ruangwa mkoani Lindi itacheza na Chipukizi na saa 2:15 Singida Big Stars FC itapambana na KMKM FC ya jijini Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news