Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Angella Muhozya akimuonesha moja ya chumba cha kulipia (VIP) Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania, Chu Kun alipotembelea taasisi hiyo hivi karibuni kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na mfumo wa umeme wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Yona Gandye akielezea huduma zinazotolewa katika chumba cha upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Cathlab) wakati Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania, Chu Kun alipotembelea JKCI kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na taasisi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt.Angella Muhozya akimuelezea huduma zinazotolewa na taasisi hiyo, Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania, Chu Kun alipotembelea JKCI kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo zinazotolwea na taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.