NA ADELADIUS MAKWEGA
WAKRISTO wametakiwa kulisoma neno la Mungu, kulichukua katika maisha yao na kuliishi huku kila Mkristo akitakiwa kuwa shuhuda kama Yohane Mbatizaji katika maisha yake yote.
Hayo yamesemwa katika misa ya Jumapili ya pili ya mwaka A wa Kanisa, Januari 15, 2023 katika Kanisa la Bikira Maria imakulata, Parokia ya Chamwino Ikulu, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
Hayo yamesemwa katika misa ya Jumapili ya pili ya mwaka A wa Kanisa, Januari 15, 2023 katika Kanisa la Bikira Maria imakulata, Parokia ya Chamwino Ikulu, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.

“Kama muumini haufanyi hivyo, basi wewe haufai kuwa mfuasi wa Kristo, lazima huyo Kristo ashuhudiwe katika maisha yako ya kila siku popote Mkristo alipo, kama wewe ni mtoto au mtu mzima, iwe nyumbani au kazini, hilo neno jema lipelekwe huko.”
Misa hiyo iliambatana na maombi kadhaa na mojawapo ni hili, “Mungu Baba utasaidia kushuhudia huruma ya Kristo hili kuwasaidia wengine wenye shida za roho na za mwili."
Wakati wa matangazo ndani ya misa hiyo Muuguzi Mkuu Christina Matias aliwaambia waamini kuwa shirika la United Missionaries ambalo huwa linahudumia wakimbizi litaanza utoaji wa chakula kwa wakazi wa Chamwino kuanzia 2023 hadi 2028.
Hadi wakati misa hiyo ya pili ya dominika hii inakamilika hali ya hewa ya eneo la Chamwino ikulu imekuwa ikipata mvua na jua , huku mazao ya wakulima wengi yakiendelea vizuri na wengine wakiendelea na upandaji.