Maono ya Prof.Muhongo yaongeza nguvu Sekta ya Elimu jimboni

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Prof.Sospeter Muhongo ameendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Shule ya Sekondari Muhoji katika Kata ya Bugwema ambapo yeye binafsi amechangia saruji mifuko 150 na kuahidi kuendelea kuchangia ujenzi huo. Huku Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt.Halfan Haule akichangia mifuko 20 ya saruji.
Harambee hiyo imefanyika Januari 24, 2023 ambapo upande wa wanakijiji wakiongozwa na Diwani wa kata, Mhe. Clifford Machumu wamechangia saruji mifuko 124.

Fedha taslimu shilingi 305,000. Ambapo michango hiyo ya wananchi ni mbali na michango yao mingine ya nguvu kazi ya kusomba mawe, mchanga, kokoto na shilingi 45,000 kwa kila kaya.
"DC wa Wilaya ya Musoma, Mhe Dkt.Halfan Haule amechangia saruji mifuko 20. Na Januari 23, 2023 alishiriki kwenye ufyatuaji wa matofali. Mbunge wa Jimbo amechangia saruji mifuko 150. Ataendelea kuchangia," imeeleza taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge Prof.Muhongo.

"Kijiji cha Muhoji ni moja kati ya vijiji vinne vya Kata ya Bugwema, vingine ni Masinono, Kinyang'erere na Bugwema. Kata hii ina Sekondari moja iitwayo Bugwema ambayo kwa sasa imeelemewa sana kwa sababu hizi," imeeleza taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge na kuongeza kuwa.
"Kidato cha Kwanza (Form I) cha mwaka huu (2023) kina jumla ya wanafunzi 362 walioko kwenye mikondo 7 ya wanafunzi 50 kwa kila mkondo. Iwapo kila mkondo ungalikuwa wa wanafunzi 40, Form I hii ingalikuwa na mikondo 9. Walimu 10 tu kwa Sekondari yenye jumla ya Wanafunzi 748.Mbali ya mirundikano hiyo kwenye Bugwema Sekondari, bado wanafunzi wa kutoka Kijiji cha Muhoji wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 24-30 kwenda na kurudu kutoka masomoni," imeeleza taarifa hiyo.
"Kuhusu malengo yaliyowekwa ni Ujenzi wa Vyumba vinne vya Madarasa vyenye Ofisi mbili (katikati) za Walimu na Choo chenye Matundu nane ukamilike kabla ya 30 Julai 2023. Muhoji Sekondari ifunguliwe Januari 2024.

"Tunakukaribisha kuchangia ujenzi wa Muhoji Sekondari. Mchango wako mpelekee kwa Mtendaji wa Kijiji (VEO), Samwel Mourice 0686 557 264 /0769 458 012. Elimu ni uchumi, elimu ni maendeleo karibu tuchangie ujenzi wa shule zetu," imeeleza taarifa hiyo.
Picha za juu zinaonesha matukio mbalimbali ya harambee ya ujenzi wa Muhoji Sekondari ya Kijiji cha Muhoji Kata ya Bugwema.Vilevile, picha mbili zinamuonesha DC Mhe. DktHalfan Haule (mwenye shati nyeupe) akishiriki kufyatua matofali ya Muhoji Sekondari. Hiyo ilikuwa Januari 23,2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news