Mshambuliaji wa kati Jean Othos Baleke kutua Simba leo

NA DIRAMAKINI

UONGOZI wa Klabu ya Simba umetangaza kukamilisha usajili mshambuliaji wa kati Jean Othos Baleke raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo kwa mkataba wa miaka miwili kutoka TP Mazembe.

Baleke (21) anatarajia kuwasili nchini leo na atajiunga na kikosi ambacho kitakuwa kimerejea kutokea Dubai.

Baleke amejiunga na Simba SC akitokea Nejmeh FC ya Lebanon ambapo alipelekwa kwa mkopo mwanzoni mwa msimu huu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Simba SC, Usajili wa Baleke ni matakwa ya benchi la ufundi ili kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji.

Baleke ni mchezaji wa tatu kusajiliwa kwenye dirisha hilo akitanguliwa na Saido Ntibanzokiza na Ismael Sawadogo aliyemtambulisha awali.

Kwa mujibu wa taratibu Baleke ataitumikia Simba kwenye mashindano yote ikiwemo Ligi ya mabingwa Afrika kwani hakucheza katika hatua za awali.

Wasifu wa mchezaji

Jina Kamili: Jean Toria Baleke Othos

Tarehe ya Kuzaliwa: Aprili 17, 2001

Umri: Miaka 21

Urefu: Mita 1,69

Uraia: DR Congo

Nafasi: Mshambuliaji wa kati

Klabu: Simba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news