NA DIRAMAKINI
HALMASHAURI ya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imepiga marufuku wanaume kusimama na wanafunzi wa kike kwa zaidi dakika 15 katika mazingira yenye mashaka.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kufanya utafiti mwepesi na kubaini kwamba kuna kundi kubwa la watoto wa kike wanaokatisha masomo kwa kupata mimba za utotoni.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mheshimiwa Andrew Tsere amesema baada ya kufika katika wilaya hiyo alibaini wanafunzi kukutana na changamoto nyingi ikiwemo ya mimba na uhaba wa walimu na kisha kuja na mpango wa elimu ya makambi na katazo la wanaume kusimama na wanafunzi katika mazingira yasiyo rafiki.
Hayo ameyabainisha kwenye kikao cha mapitio ya tathimini ya utekelezaji wa shughuli za uboreshaji na usimamizi wa elimu mkoa kilichohudhuliwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt.Festo Dugange.
Aidha, wakati Wilaya ya Ludewa ikiweka mkakati huo na kisha kuinua ufaulu kutoka asilimia 60 hadi 80 katika kipindi cha miaka mitatu,Serikali ya Mkoa wa Njombe kupitia kwa Katibu Tawala, Judica Omary imesema tatizo la upungufu wa walimu na mdondoko wa wanafunzi limekuwa kubwa hatua ambayo inamsukuma mkuu wa mkoa huo, Anthony Mtaka kuweka msimamo mpya ili kufikia malengo katika Sekta ya Elimu.
Mwaka 2018, uongozi wa Kata ya Nyehunge wilayani Sengerema ilipitisha sheria ya kuwacharaza viboko 12 au faini ya shilingi 10,000 wanaume watakaokutwa wamesimama na wanafunzi wa kike.
Sheria hiyo ndogo ilipitishwa kwenye kikao cha Maendeleo ya Kata (WODC) baada ya tatizo la wanafunzi kukatisha masomo kutokana na kupata uja uzito kuzidi kuwa sugu.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nyehunge wakati huo, Mabula Enock alisema sheria hiyo itasaidia kudhibiti vitendo vya wanaume wanaoshawishi wasichana kufanya nao mapenzi na baadaye kuwapa ujauzito unaokatisha ndoto zao.
“Tumelazimika kupitisha sheria hiyo ili kuungana na mkuu wa wilaya yetu, Emmanuel Kipole (wakati huo) aliyeagiza wanaume watakaokutwa wamesimama na wanafunzi wacharazwe viboko au kutozwa faini ya shilingi 10, 000 ama vyote kwa pamoja,”alisema.
Agizo la mkuu huyo wa wilaya alilitoa Oktoba, mwaka 2017 wakati akikaribisha wanafunzi 81 kujiunga na masomo ya kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Nyehunge.