OFISI ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu (OWM-KVAU) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), inautangazia Umma kuhusu ufadhili unaotolewa na Programu ya Kukuza Ujuzi na Stadi za Kazi kwa ajili ya Ajira zenye Tija (Education and Skills for Productive Jobs-ESPJ) ambayo inaratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) kupitia ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Dunia (WB).
Lengo la programu hii, ni kuwezesha Vijana 411 wenye Ulemavu kupata mafunzo ya ujuzi yatakayowawezesha kushiriki katika shughuli za kiuchumi kwa kujiajiri au kuajiriwa.
Mafunzo hayo ya ujuzi yatatolewa katika vyuo vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa watu wenye Ulemavu vinavyomilikiwa na Serikali.
Wanafunzi wanatakiwa kuripoti vyuoni hapo kuanzia tarehe 23 hadi tarehe 24 Januari, 2023 saa 2.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni. Masomo yataanza rasmi tarehe 25 Januari, 2023.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Mkuu wa Chuo husika.
Majina yanapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na katika Halmashauri zote nchini kupitia Mkurugenzi wa Halmashauri.
Kwa ufafanuzi na maelezo zaidi wasiliana na: Mratibu wa Vyuo vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu kwa namba ya simu: 0755906018 au barua pepe suzana.mayengo@kazi.go.tz.
Majina ya waliopata ufadhili pamoja na vyuo walivyopangiwa yameorodheshwa hapa chini: