Prof.Muhongo aendelea kuifikia shule baada ya shule jimboni

NA FRESHA KINASA.

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo anatarajia kuendesha harambee kwa ajili ya ujenzi wa maabara tatu za Shule ya Sekondari Seka iliyopo jimboni humo.

Hayo yamebainishwa leo Januari 28, 2023 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Ambapo imesema kuwa, harambee hiyo itafanyika Alhamisi ya Februari 2, 2023 kuanzia saa tatu asubuhi katika Shule ya Sekondari ya Seka katika Kijiji cha Seka.

"Seka Sekondari ni shule mpya ambayo kwa sasa ina wanafunzi wa Kidato cha Kwanza hadi cha tatu.Jumla ya wanafunzi ni 344, na walimu wapo nane. Sekondari hii ilijengwa baada ya kubaini kwamba Sekondari ya Kata (Kasoma Sekondari) ilikuwa imeelewa na wingi mkubwa wa wanafunzi kutoka vijiji vitano vya Kata ya Nyamrandirira,"imeeleza taarifa hiyo na kusema kuwa.

"Seka Sekondari haina maabara, kwa hiyo mafunzo ya vitendo yanafanyiwa kwenye chumba kimoja cha darasa.Sekondari hii inahitaji maabara tatu za Physics, Chemistry na Biology. Hivyo siku ya Alhamisi ya Februari 2,2023 muda Saa 3:00 asubuhi Seka Sekondari Kijiji cha Seka itafanyika harambee na michango ipelekwe kwa Headmaster Seka Sekondari simu. 0787 411 265,"imesema taarifa hiyo.

"Ombi maalumu,wazaliwa wa Kata ya Nyamrandirira wanaombwa sana wachangie ujenzi huu. Hao ni wazaliwa wa vijiji vya Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na Seka. Wadau wengine wa maendeleo wanaombwa kuchangia ujenzi huu ili kupata maabara tatu za Seka Sekondari, elimu ni uchumi, elimu ni maendeleo," imesema taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news