NA GODFREY NNKO
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, majaji, watumishi wa Mahakama, familia, ndugu na jamaa wote kwa kuondokewa na mpendwa wao, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa, Mheshimiwa Dkt.John Harold Kulimba Utamwa.
Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ametoa pole hizo kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii Januari 2, 2023 ikiwa ni saa chache baada ya kuripotiwa kutokea kwa kifo hicho.
"Nimesikitishwa na kifo cha Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa Dkt.John Utamwa aliyefariki Dunia leo jijini Dar es Salaam. Nawapa pole Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Majaji, watumishi wa Mahakama, familia, ndugu na jamaa wote. Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani. Amina,"ameeleza Mheshimiwa Rais Dkt.Samia.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano- Mahakama ya Tanzania, Artemony Vincent Tiganya ilieleza kifo hicho kilitokea Januari 2, 2023 wakati akiendelea na matibabu jijini Dar es Salaam.
"Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania, anasikitika kutangaza kifo cha Mhe.Dkt.John Harold Kulimba Utamwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa kilichotokea leo Januari 2, 2023 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipokuwa anapatiwa matibabu.
"Marehemu Mhe.Jaji Dkt.Utamwa amekuwa akisumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu ambapo tarehe 17 Desemba, 2022 alilazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa. Mnamo tarehe 18 Desemba, 2022 alihamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kuendelea kupatiwa matibabu hadi mauti yalipomfika.
"Marehemu Jaji Dkt.Utamwa alijiunga na Mahakama ya Tanzania tarehe 17/02/1992 akianzia ngazi Hakimu Mkazi. Alipanda ngazi mbali mbali ndani ya Mahakama na hatimaye aliteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania tarehe 24/6/2010.
"Akiwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Marehemu Jaji Dkt. Utamwa alifanya kazi katika kanda za Dar es Salaam, Tabora, Mbeya na Iringa.
"Kufuatia msiba huo, taratibu za maziko zinafanyika nyumbani kwa marehemu Madale jijini Dar es Salaam. Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitaendelea kutolewa,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.