NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa ofisi za balozi zinazowakilisha nchi zao na mashirika ya Kimataifa kuungana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhamisha ofisi zao kwenda makao makuu jijini Dodoma.
“Mnafahamu kwamba Dodoma ndiyo makao makuu rasmi ya nchi yetu na Serikali imehamia huko na tunachukua kila hatua kuhakikisha linakuwa Jiji la kisasa na huduma zote muhimu.Tunapofanya hivyo tunawaomba mfanye mipango ya kuhamia pia kwenda kwenye makao makuu ya nchi yetu ili kunufaika na misaada mbalimbali ambayo Serikali inatoa kabla ya kumaliza wakati wake;
Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ametoa rai hiyo Januari 13, 2023 katika Ukumbi wa Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiwahutubia mabalozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.
Zinazohusiana
Rais Dkt.Samia na Wanadiplomasia
Sambamba na wawakilishi wa mashirika ya Kimataifa wakiwa katika Sherehe za Mwaka Mpya (Diplomatic Sherry Party).
Pia Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amezitaka ofisi hizo kufanya mawasiliano na mamlaka husika kupewa taarifa ya fursa zinazopatikana jijini Dodoma.
Wakati huo huo, Rais Dkt.Samia amesema, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeridhia Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika (AfCFTA) na tayari imeshajipanga kuanza biashara, kuimarissha zaidi sekta ya utalii, kushiriki katika ulinzi na amani ikiwemo kudumisha umoja na mshikamano nchini.