Rais Dkt.Samia, Dkt.Mwinyi wasisitiza amani, upendo, mshikamano na kazi kwa bidii ili mwaka 2023 uwe wa neema zaidi

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa pamoja wamewataka wananchi kudumisha amani, upendo, mshikamano na kufanya kazi kwa bidii ili mwaka 2023 uwe wa neema zaidi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi, alipofika Ikulu jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu tarehe 11 Januari,2022. (Picha na Maktaba/Ikulu).

Viongozi hao wakuu wa nchi wameyaeleza hayo kwa nyakati tofauti kupitia salamu za mwaka mpya 2023 walizozitoa kupitia kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii.
"Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia kuiona siku ya leo (Januari 1, 2023) tunapoiaga 2022 na kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2023. Kama Taifa, tunaiaga 2022 tukiwa wamoja, wenye amani na tuliopiga hatua kubwa kimaendeleo.
"Tuendelee kufanya kazi kwa bidii na weledi kufikia azma yetu ya kuwa bora zaidi na zaidi. Serikali itaendelea kufanya kila litalowezekana ili 2023 kwa uwezo wa Mola, iwe ya mafanikio makubwa zaidi ya kiuchumi na kijamii kwa kila mmoja na Taifa zima. Tuwe na mwaka mwema 2023,"amefafanua Mheshimiwa Rais Dkt.Samia.

Kwa upande wake Rais Dkt.Mwinyi amebainisha kuwa, "Naungana nanyi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka zake kumaliza kwa amani mwaka 2022 na kuukaribisha mwaka mpya 2023. Tuendelee kudumisha amani, upendo, mshikamano na tuchape kazi kwa maendeleo ya Taifa letu. Heri ya Mwaka Mpya 2023,"ameeleza Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news