RC Babu atoa wito kwa wadau wa Mahakama

NA MWANDISHI WETU

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu amewaomba wadau wa Mahakama kuweka mifumo mizuri ili kuhamasisha utatatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi, kwani hakuna mkoa wenye migogoro mingi kama Kilimanjaro, hasa inayohusu ardhi.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi, Mhe. Dkt. Juliana Massabo (kushoto) akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Sheria.

“Lakini pia nitoe rai kwa watumishi na watendaji wa Mahakama kujiepusha na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa maadili na kuacha kufanya kazi kwa mazoea, wahudumieni wale wanaohitaji haki kwa weledi,”amesisitiza.

Mkuu wa Mkoa huyo amewahimiza wananchi kujitokeza katika Wiki ya Sheria ili kupata msaada na ushauri wa kisheria, hivyo kuweza kutatua migogoro inayowakabili kwa njia ya usuluhishi.

Kwa upande wake, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi, Mhe. Dkt. Juliana Massabo alisema katika Wiki ya Sheria watatoa huduma mbalimbali kwa wananchi, ambapo watumishi na wadau wa Mahakama wamejipanga vyema kutekeleza jukumu hilo.

Jaji Mfawidhi huyo amewaomba wananchi wote kwa makundi mbalimbali ya kijamii kushirikiana kwa pamoja ili kuifanya kauli mbiu ya mwaka 2023 kuwa ya vitendo kwani itasaidia kukuza amani, kupunguza mlundikano wa mashauri na kuondoa au kupunguza gharama za uendeshaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news