Serikali yaagiza walimu wapewe motisha

NA ANGELA MSIMBIRA

NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Dkt.Charles Msonde amewataka viongozi ngazi zote kutoa motisha kwa walimu ili kuongeza ari ya ufundishaji kwa watoto shuleni.

Dkt.Msonde ameyasema hayo Januari 19, 2023 jijini Mwanza kwenye kikao kazi cha mapitio ya tathmini ya utekelezaji wa shughuli za uboreshaji na usimamizi wa elimu nchini.

Amesema,imefika mahali viongozi wakatambua umuhimu wa kutoa motisha kwa walimu kwa kuwa ndio waliobeba dhamana ya malezi na ufundishaji wa watoto ambao ndio tegemeo la taifa.

Dkt.Msonde amesema, mwalimu ni mzazi wa pili kwa kuwa anakaa na watoto wakiwa na umri mdogo mpaka wanapokuwa, hivyo ni watu muhimu katika jamii ni wajibu wa viongozi kuwatunza kuwaheshimu na kuwathamini.

"Walimu wanawajibu wa kuhakikisha nidhamu, maadili,uzalendo na utanzania wa mtoto unafundishwa na kushawishi jamii juu ya jinsi gani mtoto awe, hivyo ni vyema tukatoa motisha kwa walimu nchini ili kuongeza ari ya utunzaji na ufundishaji wa watoto wetu,"amesema Dkt.Msonde.

Aidha, Dkt.Msonde ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa walimu wote nchini kujitoa kwa moyo kwenye ufundishaji wa watoto kuanzia ngazi ya awali kwa kuwa ndio wamebeba dhamana ya kumkuza mtoto kimaadili, kiujuzi na kuhakikisha anajitegemea na kuwa raia mwema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news