NA DIRAMAKINI
KIKOSI cha Simba Queens leo alfajiri kitasafiri kuelekea mkoani Iringa kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier League (SLWPL) dhidi ya Mkwawa Queens utakaopigwa Januari 11, 2023.

Kocha mkuu, Charles Lukula amesema kikosi kipo kwenye hali nzuri na morali ya wachezaji ipo juu tayari kuhakikisha wanapambana kupata alama tatu.
Lukula amesema, ushindi waliopata dhidi ya Fountain Gate siku ya Jumanne iliyopita umeongeza ari kwa wachezaji ambayo anaamini itawafanya kupata ushindi.
“Tunaondoka alfajiri kuelekea Iringa kwa mchezo wa Jumatano dhidi ya Mkwawa Queens, tunatarajia utakuwa mchezo mgumu, lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.
“Ligi ya msimu huu ni ngumu, ushindani umeongezeka kila timu imejiandaa vizuri, lakini sisi ni mabingwa watetezi, hivyo tunahitaji kufanya vizuri kwenye kila mchezo,” amesema Lukula.