Wahitimu Kidato cha Nne wenye 'pass' nne za ufaulu karibuni Chuo Kikuu Huria cha Tanzania muhula wa masomo Aprili 2023

NA DKT.MOHAMED OMARY MAGUO

AWALI ya yote tunapenda kuwapa kongole na pongezi nyingi sana kwa jitihada zenu katika masomo zilizowawezesha kuhitimu na kufuzu vizuri katika masomo yenu.
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinawakaribisha wahitimu wote waliopata Pass Nne (4) za kuanzia kiwango cha D kujiunga na Certificates za chaguo lao zinazotolewa hapa Chuoni. Certificates hizo ni:

1. Certificate in Business Administration

2. Certificate in Accountancy

3. Certificate in Procurement and Supply

4. Certificate in Hair and Beauty Therapy

5. Certificate in Youth Work

6. Certificate in Information and Communication Technology

7. Certificate in Library and Information Studies

8. Certificate in Poultry Production and Health

9. Certificate in Social Work

10. Certificate in Entrepreneurship

11. Certificate in Monitoring & Evaluation

12. Certificate in Early Childhood Care and Education

Programu hizi za Certificate husomwa kwa mwaka mmoja wa masomo ambao ni sawa na miezi tisa (9) na mara baada ya kuhitimu, mhitimu hujiunga na Diploma katika fani yake.

Wapendwa Wazazi na Wahitimu,Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kina matawi katika mikoa yote ya Tanzania Bara na katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Hiki ni Chuo Kikuu cha Serikali kilichoanzishwa kwa sheria ya Bunge namba 17 ya mwaka 1992.

Tunawaomba mfike kwenye matawi yetu kwa huduma za udahili ambazo hufanywa Bure bila ya malipo yoyote. Pia, maombi yanaweza kutumwa moja kwa moja kupitia www.out.ac.tz ukiwa popote pale nchini au nje ya nchi.

Ada ya Certificate zetu ni nafuu sana ambapo kwa mwaka mzima ni Laki Nane (800,000/=) tu. Ada hii inalipwa kwa awamu mbili, yaani 400,000/= kwa awamu moja. Pia, inaruhusiwa kusoma kwa Miaka 2 kwa ada hiyo hiyo bila nyongeza yoyote.

Wapendwa Wazazi,Tunawasihi muwalete watoto wenu Chuo Kikuu Huria cha Tanzania wapate elimu bora kwa gharama nafuu. Mtoto wako atasoma akiwa anatokea nyumbani na hivyo hakuna gharama za hosteli.

Maombi yanapokelewa sasa hivi kwa ajili ya Muhula wa APRILI 2023. Hakuna haja ya kupoteza muda kwani mwezi Aprili 2023 masomo yanaanza katika vituo vyetu vyote nchi nzima.

Kumbuka: Wahitimu wa Kidato cha Nne wa miaka ya nyuma wenye ufaulu wa Pass Nne nao pia wanapokelewa.

WENU

Dkt. Mohamed Omary Maguo

Mhadhiri na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

30/1/2023

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

Previous Post Next Post

International news