Wamsikitisha Waziri Kairuki uandikishaji wanafunzi

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Tanga kuendelea kusimamia uandikishaji kwa wanafunzi wa elimu ya awali,msingi na kidato cha kwanza.
Ameyasema hayo Januari 16, 2023 katika kikao chake maalumu alichofanya na viongozi wa elimu kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa mkoani Tanga na kusema kuwa viongozi wa mkoa wanatakiwa kuangalian njia nzuri ya kuongeza uandikishaji wa wanafunzi shuleni.

''Haiwezekani hadi leo bado kuna wanafunzi hawajaripoti shuleni, kwa kweli haiwezekani bado kuna watoto zaidi ya elfu 27 katika mkoa huu hawajaripoti kidato cha kwanza kila mmoja arudi ajitafakari na kufuatilia mtoto mmoja baada ya mwingine,"amesema Waziri Kairuki.

Ameongeza kuwa, Wilaya ya Lushoto bado ipo chini sana kwa uandikishaji ikifuatiwa na Wilaya ya Pangani pamoja na Wilaya ya Korogwe.

Pia amesema kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi bado kuna idadi kubwa ya watoto ambao hawajaripoti shuleni wakiwa na asilimia 11 huku Korogwe Mji wakiwa asilimia 22.78.

Waziri Kairuki amewataka viongozi wa wilaya zote za Mkoa wa Tanga kujitathimini kwa kuwa hali ya uandikishaji wa wanafunzi kwenye ngazi zote bado hairidhishi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news