Waziri Simbachawene:Mungu atuongoze 2023 ili tuendelee kuenzi na kudumisha tunu za taifa letu

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe.George Simbachawene ameomba wananchi kuendelea kuiombea nchi dhidi ya majanga mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukame, njaa, mafuriko na ajali.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiwa katika mkesha wa kitaifa wa dua maalum kwa taifa la Tanzania.

Kauli hiyo Desemba 31, 2022 ameitoa kwenye mkesha wa kitaifa wa dua maalum kwa taifa la Tanzania ambao umetumika kuuaga mwaka 2022 na kuukaribisha mwaka 2023 uliofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

“Tumuombe Mungu kwa Mwaka 2023, ili tuendelee kuenzi na kudumisha tunu za taifa letu za amani, umoja, mshikamano, utu, haki, heshima ya mwanadamu, uhuru na demokrasia.”

Waziri Simbachawene amehimiza kuendelea kuimarisha ulinzi wa mipaka ya nchi yetu, watu wake na usalama wa mali zao, ikiwa ni pamoja na kuwa na Serikali madhubuti, inayosikiliza na kutekeleza matakwa ya wananchi kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi.

“Tuwaombee viongozi wetu wakuu, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar afya njema na nguvu ya kutosha kuendelea kuisimamia miradi ya kimkakati kwa ufanisi kama ilivyokuwa kwa mwaka 2022 ili iweze kukamilika katika wakati uliopangwa.”

"Aidha, tuiombee mihimili ya Bunge na Mahakama pamoja na viongozi wake kuendelea kutekeleza majukumu yake ya kutunga sheria, kuisimamia serikali na kutafsiri sheria ipasavyo.

“Tuwaombee watoto wetu ambao kimsingi ndiyo taifa la kesho dhidi ya mmomonyoko wa maadili; ukatili, ambao unaoendelea kushamiri katika ngazi za familia, shuleni na jamii kwa ujumla,” amesema Waziri Simbachawene.

Mwenyekiti Mkesha Mkuu wa Dua Maalum kwa Taifa la Tanzania, Mkoa wa Dar es Salaam, Mchungaji Derrick Luhende akimkaribisha Waziri alitumia Kitabu cha 1Tiomotheo 2:1..Basi, kabla ya mambo yote nataka dua na sala na maombezi shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka tuishi maisha ya utulivu na amani katika utauwa wote na ustahimilivu hili ni zuri nalo linakubalika mbele za Mungu mwokozi wetu ambaye hutaka watu wote waokolewe na kutaka kujua yote yaliyo ya ukweli.

“Amani na Utulivu endelevu tunayoifurahia katika taifa letu ni zawadi kutoka wa Mungu pekee, ni fursa ambayo sio ya kuichukulia kirahisi.”

Aidha, maombi haya tumefanikiwa mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, mapambano dhidi ya Uviko, Mungu ametusaidia kuongezeka kwa nidhamu ya Utumishi wa Umma.

“Tunampongeza Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Mpango mkakati wa kuitangaza Tanzania kupitia Royal Tour ambao unaifanya Tanzania kuwa kivutio kikubwa cha Utalii uliwenguni.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news