NA GODFREY NNKO
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Dkt.Angeline Mabula amesema, wizara hiyo ipo katika utekelezaji wa mipango thabiti itakayowawezesha kuwa na usimamizi bora wa ardhi kwa maendeleo endelevu ya biashara na uwekezaji katika kukuza uchumi nchini.
"Wizara yangu inaendelea na maboresho ya kisera, kisheria na kiutendaji katika Sekta ya Ardhi ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.
"Aidha katika mkutano huu tunatarajia kupokea maoni, hoja na mapendekezo zaidi yatakayotuwezesha kuwa na usimamizi bora wa ardhi kwa maendeleo endelevu ya biashara na uwekezaji katika kukuza uchumi nchini;
Ameyasema hayo Februari 14, 2023 wakati akifungua Mkutano wa Pili wa Wadau wa Sekta ya Ardhi nchini katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo wa pili, umeongozwa na kauli mbiu ya "Usimamizi bora wa ardhi kwa maendeleo endelevu ya biashara na Uwekezaji nchini".
Pia Waziri Dkt.Mabula amezikumbusha mamlaka zote za upangaji nchini kutenga ardhi kwa ajili ya uwekezaji. "Na tukumbuke Mheshimiwa Dkt.Samia Suluh Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefungua milango kwa ajili ya Uwekezaji, Sekta ya Kilimo, Viwanda na nyinginezo zinahitaji kuwa na ardhi.
"Hivyo nashauri pamoja na kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji ni vyema maeneo hayo yakatwaliwa na kuwa tayari ili kuepuka usumbufu pale anapopatikana mwekezaji, kwa maeneo ya vijiji taratibu za uhaulishaji zifanyike mapema ili kuondoa usumbufu pale kijiji kinapopata mwekezaji,"ameagiza Waziri Dkt.Mabula.
Amewaeleza wadau hao kuwa, maoni, hoja na mapendekezo yao yatasaidia pia katika mpango wa bajeti wa mwaka 2023/2024.
"Kwa hiyo kikao hiki kimekuja wakati mwafaka tunaelekea pia katika uandaaji wa bajeti ya 2023/2024, kwa hiyo kila wazo mtakalolitoa ambalo linakwenda kuboresha sekta husika tutalipa kipaumbele ili kile tunachokwenda kukiandaa kiwe kinatokana na wadau wa ardhi kama nyie ambao mmefika hapa,"amesisitiza Mheshimiwa Waziri Dkt.Mabula.
Waziri Dkt.Mabula amefafanua kuwa,lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hasssan ni kuona Sekta ya Ardhi inachangia kwa kiasi kikubwa katika suala zima la kujenga uchumi wa taifa.
"Kwa hiyo tukiweza kushiriki kikamilifu na kutoa sapoti tutakuwa tunamuunga mkono kwa kasi kikubwa Mheshimiwa Rais ambaye anaiona sekta hii kama wezeshi kwa maana ya kwamba sekta nyingine zinategemea mipangilio mizuri ya Sekta ya Ardhi.
"Tukishindwa kupanga vizuri na kuweka mipango inayoeleweka maana yake tunakwamisha wengine pia. Sekta hii ni kuona kwamba inachangia kukuza uchumi kwa kuitumia ardhi kama mtaji, kama mali, lakini kama sehemu ya kila hatua ya maendeleo inategemea sekta hii iwe mfugaji, mkulima, mchimba madini bado unategemea sekta hii,"amesisitiza Waziri Dkt.Mabula.
Migogoro
Mbali na hayo, Mheshimiwa Waziri Dkt.Mabula akizungumzia utatuzi wa migogoro ya ardhi amesema,kwenye eneo hili, wizara imeendelea kushirikiana na wizara zikiwemo taasisi zingine za umma kuhakikisha wanashughulikia migogoro iliyopo na kudhibiti migogoro mipya isijitokeze.
Miongoni mwa mikakati waliyonayo, Waziri Dkt.Mabula amesema ni pamoja na kuendelea kuhama kutoka mifumo ya analojia kwenda digitali, kuongeza kasi ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi kupitia miradi ya KKK.
Pia kutekeleza miradi ya urasimishaji na miradi mingine inayotekelezwa na wizara, kuendelea kukutana na wadau wa sekta ili kubainisha changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.
Sambamba na kuwa na timu ya kisekta inayoendelea kusikiza kero, malalamiko na kuitatua. Nyingine ni kuendelea kuwa na kliniki za kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi na kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari na machapisho kuhusu majukumu ya wizara, haki na wajibu wa mwananchi kwenye masuala ya ardhi.