Benki Kuu ya Tanzania yashinda Tuzo ya Uzingatiaji wa Sheria, Miongozo na Kanuni za Serikali Mtandao

NA MWANDISHI WETU

BENKI Kuu ya Tanzania imeibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha ‘Uzingatiaji wa Sheria, Miongozo na Kanuni za Serikali Mtandao’.
Tuzo hiyo kwa BOT imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma, Mhe. Deogratius Ndejembi, tarehe 8 Februari 2023 jijini Arusha kwenye kikao kazi cha 3 cha Serikali Mtandao kilichoandaliwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA).

Kikao kazi hicho kimewakutanisha watumishi wa umma na wadau wengine kutoka taasisi mbalimbali za Serikali kujadili juu ya mafaniko na changamoto za utekelezaji wa serikali mtandao (matumizi ya TEHAMA serikalini) kikiwa na kauli mbiu ya “Mifumo Jumuishi ya TEHAMA kwa utoaji bora wa huduma za umma”. Aliyepokea tuzo hiyo kwa niaba ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ni Meneja Idara ya Uundaji na Usimamizi wa Mifumo, Bw. Christopher Nyato.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news