Benki ya Dunia kuwapiga jeki ma-hustlers wa Kenya

NA DIRAMAKINI

BENKI ya Dunia imeahidi kuunga mkono Hustler Fund (Mfuko mahususi kwa ajili ya kusaidia watu maskini nchini Kenya) ili kuinua kundi lililo hatarini zaidi kiuchumi nchini Kenya.

Wakati wa kampeni zake kupitia uchaguzi uliopita,Mheshimiwa William Samoei arap Ruto alisisitiza kuwa, atawawakilisha raia maskini nchini humo (hustlers) ambao, alidai walipuuzwa na serikali za awali kwa misingi kwamba wao maskini hawakuwa na lao katika nchi ya Kenya.
Picha na Ikulu.

Ahadi hiyo imetolewa hivi karibuni wakati wa mkutano wa mashauriano kati ya Rais Ruto na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Victoria Kwakwa katika Ikulu ya Nairobi.

Bi.Kwakwa alisema, benki hiyo itatoa msaada wa kiufundi na kifedha kwa Hustler Fund. "Benki inashirikiana sana na programu na mpango unaowawezesha maskini na walio hatarini zaidi. Tutaleta mezani njia za kutoa usaidizi wa usalama kwa watu hawa,”alisema.

Pia Bi.Kwakwa alisema, benki hiyo itaunga mkono mipango ya nchi dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Rais Ruto alikiri kuridhika na mchango muhimu wa kiuchumi ambao unatekelezwa na benki hiyo katika maendeleo ya nchi.

Rais aliitaka, benki hiyo kuongeza uwekezaji katika mipango ya kuongeza tija katika kilimo akisema serikali inashughulikia ujenzi wa mabwawa na ruzuku ya mbolea miongoni mwa mengine. "Tunatarajia msaada wenu katika ajenda yetu ya maendeleo,"alisema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news