Changamoto ya umeme, ubovu wa barabara wakitatiza Chuo cha Afya cha KAM

NA MWANDISHI WETU

CHUO cha Afya cha KAM kilichopo Kimara Korogwe jijini Dar es Salaam kinakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo kukatika kwa umeme jambo ambalo haileti tija kwa chuo hicho
Hayo yamebainishwa leo na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Jennifer Domínick wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wilayani Ubungo walipotembelea chuoni hapo kuangalia huduma mbalimbali zitolewazo chuoni hapo.

Dominick amesema kuwa, kukatika katika kwa umeme mara kwa mara chuoni hapo kumekuwa ni tatizo ambalo linakwamisha jitihada za chuo hicho pamoja na hospitali iliyopo chuoni hapo kwa kuwa mahitaji ya umeme ni makubwa kutokana na huduma zitolewazo.
Aidha, ametaja changamoto nyingine kuwa ni ubovu wa barabara inayoingia chuoni hapo kwa kuwa chuo hicho kina hospitali kubwa inayotoa huduma za uzazi.

"Hiki chuo ni kikubwa na kina hospitali kubwa inayotoa huduma mbalimbali ikiwemo masuala ya uzazi, fikiria mama mjamzito ameshikwa na uchungu halafu barabara yenyewe ni mbovu jambo ambalo linaweza kuhatarisha afya ya mama na mtoto aliyepo tumboni,"amesema Dominick.

Domonick ameziomba mamlaka husika kuwasaidia kutatua changamoto hizo ili chuo hicho kiweze kutoa huduma nzuri kwa manufaa ya watanzania.
Aidha amewataka watanzania kuwapelekea vijana wao kujiunga na chuo hicho. Kwa upande wake Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo, Juma Shabani ametoa rai kwa wanasiasa kutumia majukwaa kwa ajili ya kuwaelewesha wananchi wa Ubungo ambao vijana wao bado wanahitaji elimu kujiunga na chuo hicho kutokana na ubora wa elimu inayotolewa na unafuu wa gharama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news