NA DIRAMAKINI
MWENDO kasi umetajwa kuwa, chanzo kikuu cha ajali iliyosababisha vifo vya watu 12 na kujeruhi 63 katika Kata ya Pandambili Kijiji cha Silwa wilayani Kongwa karibu na Barabara ya Dodoma kwenda Morogoro.
Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia Februari 9, 2023 wilayani Kongwa mkoani Dodoma ikihusisha lori lenye namba za usajili T 677 DVX na basi la abiria la Kampuni ya Frester lenye namba za usajili T 415 DPP lililokuwa likitokea Bukoba kwenda jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Kamishna Awadh Haji ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa basi kutaka kulipita gari la mbele bila ya kuchukua tahadhari na kugongana na lori lililokuwa limebeba saruji.
Mheshimiwa Rosemary Senyamule ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amesema kuwa, ajali hiyo imehusisha magari mawili na kusababisha vifo vya watu 12 ambapo kati yao ni wanaume wanane, wanawake wanne na majeruhi 63 huku wanaume wakiwa 40 na wanawake 23.
“Serikali ilikuwa na nia njema ya kuruhusu vyombo vya usafiri kutembea usiku, lakini sasa baadhi ya madereva wanaanza kutozingatia sheria za usalama barabarani, tutaendelea kuwachukulia hatua kali,"amesema RC Senyamule.
Aidha, majeruhi wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma na Kituo cha Afya Gairo mkoani Morogoro. Pia, miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mkoa wa Morogoro na majeruhi wawili wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo.
"Nawapa pole wafiwa waliopoteza jamaa zao katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Silwa, Dodoma usiku wa kuamkia leo Februari 9, 2023 na kusababisha vifo vya watu 12. Mungu awarehemu Marehemu wote. Naviagiza vyombo vya dola kuongeza usimamizi wa sheria za usalama barabarani;
Tazama orodha ya majina hapa chini majeruhi waliopo Morogoro;
Vifo 12
ReplyDeleteMajeruhi 63
Jumla 75
Haya mabasi yanajaza abiria kupitiliza, hatuna basi za mikoani inaweza kubeba idadi hiyo
Halafu njiani Kuna check points nyingi zisizo na tija
Usiku wanajaza Sana hadi kwenye zile koridor Mana wanajua askari usiku hawakagui
ReplyDeleteKaribia mabasi mengi ya mikoani watu wanasimama utakuta wengine wanachuchumaa
ReplyDeleteKweli kabisa wanasema wanaongeza Posho zao
ReplyDeleteWanaweka kwenye koridi vigoda magari mengi jamani wakuwabana ni Dereva na Kondakta wanagawana pesa za vigoda na vindoo vidogo abiria hana sauti kabisa wakomeshwe wahusika dereva na utingo wake na abiria tupige simu walizotuwekea ndani ya bus tena nyuma ya dereva
ReplyDeleteKama viongozi wanasikia,tupo wazalendo tunaoweza kusafiri kwenye hayo mabasi na tukawaripot inapotokea.
ReplyDeleteAbiria wanateseka na hawana la kufanya.inaumiza sana
ReplyDeleteHata safari za usiku zipigwe marufuku ikifika saa kumi ba mbili au linapoishia giza magari yasimame mpaka saa 11 alfajiri atakaye vunja masharti hayo achukuliwe hatua jamani ajali nyingi ni usiku hata za daa Moro sikome usiku
ReplyDeleteHii saa 1 mpaka saa 4 eti Dar Moro aaa mmm zisiwepo tutazoea tu
ReplyDelete