China kujenga sanamu ya Baba wa Taifa katika Makumbusho ya Taifa

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa amesema, China itajenga sanamu ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Makumbusho ya Taifa.
Ujenzi huo, Mheshimiwa Waziri Mchengerwa amesema ni sehemu ya kumuenzi Kiongozi huyo ambaye alikuwa muasisi wa Taifa la Tanzania.

Mheshimiwa Mchengerwa ameyasema hayo alipokutana na Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian katika Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Amesema, Wachina watajenga sanamu hiyo kwa gharama zao wenyewe kama sehemu ya kuimarisha ushirikiano wa miaka mingi kati ya Tanzania na China.

Naye Balozi wa China Nchini Tanzania, Chen Mingian amesema sanamu hiyo itawekwa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam ifikapo mwezi Machi, mwaka huu.

Pia amesema kwamba, nchi yake inathamini sana mchango mkubwa alioutoa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kuunganisha Taifa la Tanzania na kujenga mahusiano imara na nchi ya China.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news