NA MWANDISHI WETU
MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu ameongoza zoezi la upandaji miti katika Kijiji cha Ijoka katika Kata ya Mpombo Halmashauri ya Busokelo ikiwa ni hatua muhimu ya kulinda vyanzo vya maji, kudumisha uoto wa asili na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, Haniu ameagiza wakazi wa eneo hilo kuhakikisha wanapanda miti mara kwa mara sambamba na kuepukana na tabia ya ukataji miti hovyo, kuchoma moto, kulima kando ya vyanzo vya maji na kuchunga mifugo kwenye hifadhi za maji.

"Niagize kila kata kuwe na ratiba maalumu inayoonesha ni lini mbolea inaletwa katika kata husika ili kuwaondolea adha wananchi kufuata huduma umbali mrefu huku wakipoteza muda mwingi wa uzalishaji,"ameagiza Haniu.

Katika hatua nyingine Haniu ametoa maelekezo kwa wazazi wote kuhakikisha watoto wao waliofikisha umri wa kwenda shule sambamba na kujiunga na kidato kwanza wanawapeleka mapema kwani kufanya hivyo itasaidia kupata huduma hiyo muhimu kwa ustawi wa mtoto.