Domenico Tedesco arithi mikoba ya Roberto Martinez

BRUSSELS-Shirikisho la Soka nchini Ubelgiji (RBFA) limesema Domenico Tedesco anachukua nafasi ya kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ubelgiji.

Tedesco mwenye umri wa miaka 37 mzaliwa wa Italia anarithi mikoba ya Roberto Martinez, ambaye alijiuzulu baada ya Ubelgiji kushindwa kufuzu kwa hatua ya mtoano kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar 2022.

"Kwangu mimi ni heshima kubwa kuwa kocha mkuu mpya wa Ubelgiji. Ninasubiri kwa hamu kazi hii na nina ari kubwa. Nilifarijika tangu mazungumzo ya awali," Tedesco alieleza kupitia tovuti ya RBFA.

Uteuzi huo ulitarajiwa tangu mwishoni mwa Januari, mwaka huu. Ingawa, ucheleweshaji huo ulisababisha kushukiwa kuwa Tedesco alikuwa akizingatia kazi iliyokuwa wazi ya Hoffenheim.

Dakika 15 tu baada ya tangazo la RBFA, klabu hiyo ya Bundesliga ilituma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa imemwajiri Pellegrino Matarazzo.

Mhispania Martinez aliondoka Ubelgiji baada ya kuondolewa katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia nchini Qatar, ambayo huenda ikaashiria mwisho wa "kizazi cha dhahabu" cha nchi hiyo.

Kikosi cha Ubelgiji kilichokaribia kutwaa taji kikiundwa na Kevin De Bruyne, Romelu Lukaku, Thibaut Courtois, Jan Vertonghen na Eden Hazard, miongoni mwa wengine, chini ya Martinez kilikuwa nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia la 2018. Hazard alitangaza kustaafu kimataifa baada ya Kombe la Dunia.

Picha na EuroFoot.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news