MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Serikali imesogeze mbele uwasilishaji wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ambao ulipangwa kuwasilishwa katika Bunge linaloendelea ikiwa ni sehemu ya miswada ya mabadiliko ya sheria mbalimbali.Kwa taarifa hiyo, muswada huo sasa utawasilishwa katika Bunge la Bajeti linalotarajiwa kuanza mwezi Aprili, mwaka huu.