NA DIRAMAKINI
KWA mujibu wa Serikali, faida za Mwenge wa Uhuru Kitaifa na Kimataifa ni pamoja na kuendelea kuhamasisha ari ya wananchi kujitegemea na kuwekeza katika maeneo mbalimbali katika Taifa letu.
Aidha, Kimataifa Mwenge wa Uhuru umeendelea kusimamia dhana na maudhui yake ya kumulika hata nje
ya mipaka yetu kwa kuwa msuluhishi wa amani katika Bara la Afrika na
mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine ya Afrika duniani kote. Umoja,
mshikamano, upendo na ukarimu wa Watanzania ni matunda pia ya Mwenge wa
Uhuru.
Kutokana na faida na mafanikio makubwa
yanayopatikana kupitia mbio za Mwenge wa Uhuru, Serikali inaamini kuwa
zipo faida za kuendelea kukimbiza Mwenge huo wa Uhuru.Dhana hii ni endelevu na itaendelezwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa kusisitiza misingi hiyo
bila kuchoka.