HONGERENI MHESHIMIWA BALOZI DKT.CHANA NA YAKUB


Februari 14,2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ambapo amemuhamishia, Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii huku Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii akihamishiwa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo.

Rais Dkt.Samia pia amemuhamishia Dkt.Hassan Abbas Said, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii akichukua nafasi ya Profesa Eliamani M. Sedoyeka.

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Said Othman Yakub kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo akichukua nafasi ya Dkt.Hassan Abbas Said. Kabla ya uteuzi huo, Yakub alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. DIRAMAKINI inawataki Mheshimiwa Balozi Dkt.Chana na Dkt.Yakub kila la heri katika majukumu yao mapya.

Tunaamini, imani iliyooneshwa kwenu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia itakewenda kufungua milango na fursa zaidi kwa vijana, ikizingatiwa kuwa hii Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imekuwa lango kuu la vijana kutoka na kuziendea ndoto zao. HONGERENI BALOZI DKT.CHANA NA YAKUB.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news