IJP Wambura asisitiza umuhimu wa fidia kwa wafanyakazi

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IJP Camillus Wambura amewataka watendaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kuwajengea uelewa makamanda wa polisi wa mikoa ili waweze kuelewa majukumu yao ni nini pale wanapohitaji taarifa kwa ajili ya kutoa fidia kwa wafanyakazi wanapoumia wakiwa katika kutekeleza majukumu yao.

IJP Wambura amesema hayo wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili kilichohusisha makamanda wa Polisi wa mikoa katika Shule ya Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo makamanda hao wametakiwa kudumisha uhusiano na mashirikiano kati ya Jeshi la Polisi na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Dkt. John Mduma, amesema mfuko wa fidia kwa wafanyakazi umeanzishwa kwa mujibu wa sheria na lengo kuu la mfuko huo ni kulipa fidia kwa mfanyakazi au kumsaidia baada ya mfanyakazi kuumia au kufariki dunia.

Aidha, Dkt.Mduma amesema mfuko umewekeza katika kujenga ushirikiano na uhusiano wa kimkatakati na taasisi mbalimbali zilizopo ndani na nje ya nchi sambamba na kuimarisha ushirikiano ambao umewezesha ubadilishanaji wa taarifa na uzoefu kwa lengo la kuongeza ufanisi wa kiutendaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news