JE, UPO KUNDI GANI KATI YA HAYA?

NA MWANDISHI MAALUMU

KUNA makundi manne (4) ya watu wanaotengeneza pesa hapa duniani.

1. WAAJIRIWA

Hawa ni watu ambao kimsingi wanauza muda wao almost wote wa siku nzima kwa mwajiri wao na yeye anawalipa pesa kwa kuwaambia cha kumfanyia.

Kwa kuwa kanuni ya mshahara huwa ni kumlipa mtu asilimia 10 ya anachozalisha hasa kwa makampuni makubwa basi haitakaa itokee mwajiriwa kulingana kipato na mwajiri wake.

Na hivyo wengi wa waajiriwa hufa maskini na watoto wao pia kuanza kutafuta maisha kivyaovyao kwa kusoma na kuja kuajiriwa pia hivyo hivyo.

Usikubali kubaki kwenye ajira unalipwa laki 5 kwa mwezi sawa na shilingi 1,850 yaani chini ya dola moja kwa saa.

Ina maana umesoma mpaka chuo kikuu halafu thamani ya lisaa lako moja ni less than $1!!!!? Ndiyo maana watu wengi waliosoma sana huwa hawawezi kuwa matajiri kwa sababu wanauza muda wao kwa "bei chee" halafu siku zinazidi kuyoyoma haoni mafanikio.

Huku tena ana mkopo wa gari nk. Makato na marejesho... Kwa nini usife masikini kwa style hiyo?.

2. WALIOJIAJIRI

Hawa hujitambua kidogo na kuamua kufanya kazi binafsi au kufungua biashara ndogo kama duka nk.

Lakini kwa kuwa hawana pesa ya kununua muda wa watu wengine na kuwaajiri hawa nao huwa busy kutwa kucha bila mafanikio ya maana.

Ana duka miaka 15 sasa halijawahi kupanuka likawa supermarket. Na mara nyingi huyu mtu akifa na biashara yake nayo humfuata.

Ndiyo watu wanasingizia eti alikuwa na biashara za "uchawi". Kumbe shida ni kuwa kila kitu kilikuwa kinamtegemea yeye.

3. WAMILIKI WA BIASHARA KUBWA

Hawa huwa na kipato endelevu (residual income) maana amemunua muda wa watu weeengi kawaajiri halafu kawapa majukumu kwa hiyo awepo asiwepo pesa inaendelea kuingia kwake.

Mfano kina Bakhressa, Mengi, Dewji, etc. Majina yao yanajulikana. Ni wachache nchi hii. Ukihesabu vidole vyako vya mikono na miguu majina yataisha kabla hujamaliza kuhesabu.

4. WAWEKEZAJI

Hawa ni watu wenye pesa nyingi zaidi na wana uwezo wa kuiwekeza mahali hata nje ya nchi ikawa inawazalishia pesa zaidi bila wao kuwepo kabisa. Hawa hata majina huwa hawajulikani.
Wafanyakazi kiwandani wakitengeneza mashati nchini Ghana.(Picha na World Bank/Dominic Chavez).

Kwa hiyo nadhani tayari wewe unajua kundi lipi upo (ama kama wewe ni mwanafunzi unaweza kuona kundi lipi unaelekea).

SASA SIKIA...

Makundi mawili ya kwanza ni makundi ya watu maskini. Mfano waajiriwa ni watu wanaotumia muda wao na nguvu na maarifa yao yote (waliyoyakusanya kwa miaka mingi ya kusoma kwa shidashida) kumtajirisha mtu kwa malipo kidogo yanayomwezesha huyu muajiriwa kulipa kodi (siyo kujenga), kula, kuvaa, kusafiri kwenda na kurudi kazini nk.

Yaani basic needs tu. Maisha ya waajiriwa wengi yanafanana. Mfano ni wachache sana katika ajira ambao wamejenga nyumba zao binafsi kwa hela halali ya ajira.

Kama vile ilivyo vigumu kwa mwanafunzi kwenda chuo kwa gari lake mwenyewe alilonunua kwa pesa yake halali. Wapo wachache sana.

Na hivyo hivyo waajiriwa kumiliki nyumba. Wengi wamepanga. Jiulize lini utafikia hizi level especially kama utang'ang'ania ajira tu bila kujishughulisha na kitu kingine cha ziada mpaka uzeeni? Ndiyo unastaafu unapewa kiinua mgongo lakini miaka 7 tu baada ya hapo unakufa kwa pressure.

Kwa sababu ndiyo unaanza kuona wengine wa umri sawa na wewe wako mbaaaali kimaisha hapo nguvu za kuhimili mikikimikiki ya biashara huna tena watoto na wajukuu hawana future unaanza kupata stress.

Kisa ulikuwa ungependa kiyoyozi cha kazini. Haya, endelea kufurahia kiyoyozi ndugu. Halafu mi huwa nashangaa..yaani unajua kabisa hapo kazini kuanzia kiti, dawati, computer, kalamu, karatasi, kula kitu si cha kwako. You are just hired to use them to produce for someone else. Hebu tufunguane macho leo..

Waliojiajiri nao wako busy. Kama ana duka basi kufuata mzigo yeye (hamwamini mtu), kuuza yeye, usafi yeye, kuhesabu stock yeye, ulinzi wa duka yeye ndiye analinda maana analala humo humo.

Kama jongoo alivyo na miguu mingi,lakini spidi "kiduchu" ndivyo na huyu nae. Miguu mingi ya jongoo bila macho is equal to ZERO.

Na hivyo hivyo shughuli nyingi bila maarifa is uqual to ZERO. Yaani yuko busy kila saa lakini spidi ya mafanikio ni ndogo kweli kweli.

Sasa maendeleo hayaji kwa style hiyo ila kwa kuwa hajui anahisi siku moja na yeye atakuwa kama Bakhressa. Kwani Bakhressa ndo anauza ice cream za Azam? Hujiulizi?.

KWA WANAFUNZI

Bahati mbaya sana kama ni mwanafunzi uko sekondari au chuo hiyo ndiyo ramani ya future yako. Fikiria sasa itakuwaje.

HATA HIVYO... kuna njia ya kukusaidia kuweza kuhama kutoka makundi hayo mawili kwanza na kuingia makundi mawili ya mwisho hapo juu.

Cha msingi ni Wewe kujishusha tu na kukubali kuwa unahitaji kujifunza hivi vitu. Lakini ukifikiri kuwa unajua kila kitu kuna maarifa utayakosa simply kwa kutothamini mawazo ya wengine ambao huenda ni Mungu tu anawaleta ili kukustua kidogo upate ufahamu fulani.

Kama umeajiriwa na unasoma ujumbe huu hebu jiulize ajira yako ikiisha leo ghafla PAAP!! Utaanzia wapi? Kama utaandika CV tena basi kubaliana na hali halisi tu kuwa wewe ni maskini.

Huna cha kuuza kupata pesa zaidi ya muda wako. Kumbuka rasilimali ambayo Mungu aliwagawia wanadamu wote sawa ni MUDA. 24 hours kwa kila binadamu.

Matajiri wananunua muda wewe unauuza. Yaani unafanya opposite na wanachofanya matajiri halafu unasema unataka kuwa kama wao.

Unanielewa? Kuna mtu maarufu duniani anaitwa William Gates III au kwa jina maarufu Bill Gates, anasema, "KAMA ULIZALIWA MASKINI HILO SIYO KOSA LAKO ILA UKIFA MASKINI HILO NI KOSA LAKO". Jifunze.

Kuna tajiri mwingine anaitwa JACK MA huyu ni mmiliki wa ALIBABA. Yeye anasema hatua kuja duniani kufanya kazi tu mpaka siku ya kufa bali tulikuja kuishi maisha yetu.

Anasema kuifanya kazi tu mpaka mwisho wa maisha yako utakuwa hujawahi kuishi maisha yako.

Anasema siri ya mafanikio ni kutafuta kazi ambayo utaifanya kwa miaka mitano kisha iwe imekupa pesa za kuishi maisha yako. Tafuta mpaka upiate. Kama hujaipata tafuta tu. Kama bado hujaipata watafute waliokwishaipata.

Unaona mawazo hayo?

Na kama wewe ni mwanafunzi hii ni habari njema sana maana ukiamua kujifunza vitu hivi sasa hivi ukavifanyia kazi, then I assure you miaka miwili au mitatu mbeleni wakati wenzako wanasambaza CV kuomba ridhaa ya kuingia kundi la kwanza la umaskini wewe utakuwa unanunua gari lako la pili au hata kiwanja na huenda umeanza kujenga kulingana tu na ndoto zako ni zipi.

Sababu zinaowafanya watu wengi kutofanikiwa ni pamoja na kupoteza muda mwingi kujadili vitu visivyo na tija maishani mwao hasa kwenye mitandao ya kijamii mfano sijui wimbo wa Snura, gari la Diamond, maisha ya Wema Sepetu, mambo mengi ya siasa ambayo kila siku ni mapya, matokeo ya mpira nk.

Katika kitu ambacho Mungu alitupa wote sawa ni muda. Jinsi Unavyotumia muda wako ndo inaamua hatma ya maisha yako. Huwezi kufanikiwa maishani kama muda wako mwingi ni kujadili vitu visivyo na tija maishani mwako.

Unasahau kuwa una mshahara mdogo haukutoshi hata kufanya chochote hilo ndo jambo la wewe kufikiria na kujadili. Unaishi nyumba ya kupanga hujui lini utapata walau kiwanja uanze ujenzi nk.

Una watoto au utakuwa nao siku moja wataishi kama watu au kwa kubahatisha bahatisha tu kama vile hukuwahi kuwatangulia duniani.

Ukiwaza haya mambo huwezi poteza muda kujadili Simba na Yanga au Sijui nani kapewa Wizara ya Mambo ya ndani. Aisee. Time is money my friend.

Waingereza wanasema LIFE BEGINS AT 40. Yaani maisha huanza ukiwa na miaka 40. Kwa maana kwamba ukiwa na umri huo hutakiwi kuwa unawaza ada za watoto zinatakiwa ziwepo ulishatafutaga siku nyingi ukiwa na miaka 20-39.

Wakati ukifika miaka 40 unapaswa uwe na nyumba gari urithi kwa familia yako biashara zilizosimama nk. Siyo ndo unaandika CV kuomba kazi ya tatu ili kuongeza kipato.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news