JKT:Waombe radhi na kuondoa picha mara moja

NA DIRAMAKINI

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limesikitishwa na taarifa iliyosambaa mitandaoni kwamba vijana wake 147 wana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na kuambatanishwa na picha za vijana wengine wanaohudhuria mafunzo ya JKT katika makambi.

Hayo yanajiri ikiwa Februari 3, 2023 taarifa ya Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi kwa kipindi cha Februari 2022 hadi Februari 2023 iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma ilieleza kuwa, vijana 147 kati ya 67,299 waliojiunga Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria walikutwa na maambukizi ya VVU.

Aidha, takwimu hizo ni sawa na asilimia 0.22 ya vijana waliomaliza kidato cha sita nchini na ambao waliitwa kujiunga na JKT katika kipindi cha miaka ya 2019, 2020 na 2021.

Mkuu wa tawi la utawala wa JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena amewaeleza waandishi wa habari leo Februari 6, 2023 jijini Dodoma kuwa, taarifa zilizotolewa na kamati ni sahihi, lakini wamesikitishwa kutumika picha ambazo sio za wahusika.

Brigedia Jenerali Mabena amesema, picha hizo zimeleta taharuki kwa familia za vijana wanaopatiwa mafunzo kwamba wameathirika na maambukizi ya VVU.

“Vijana ambao hukutwa na changamoto ya kiafya hufanya mafunzo yao chini ya uangalizi wa wakufunzi ili kuhakikisha wanamaliza mafunzo yao salama. JKT inavitaka vyombo vyote vya habari na mitandao ya kijamii kuomba radhi na kuondoa picha hiyo mara moja,”amesebainisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news