NA MWANDISHI WETU
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limekamata magunia matano ya bangi yenye uzito wa kilo 250 zikiwa tayari kuingizwa sokoni.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,ACP Justine Masejo wakati akitoa taarifa kuhusiana na operesheni mbalimbali ambazo wanazifanya mkoani humo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.
Kamanda Masejo amesema kuwa,Februari 2, 2023 muda saa 03:00 asubuhi huko katika Kijiji cha Kisimiri Juu Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Jeshi la Polisi mkoani humo lilifanya operesheni ambayo ilifanikisha kukamatwa kwa magunia hayo ya bangi na kuteketeza hekari saba za mashamba ya bangi.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi mkoani humo limetoa wito kwa watu wachache wanaojihusisha na matukio ya uhalifu kuacha mara moja, kwani wataendelea kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria kwa wote watakaobainika.

Tags
DCEA
Habari
Jeshi la Polisi Tanzania
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)