Kocha Mkuu wa Simba asema kesho atalia mtu

NA DIRAMAKINI

KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Roberto Oliviera (Robertinho) amesema, benchi la ufundi limewasisitiza wachezaji kuhusu umakini katika muda wote dakika 90 kwenye mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers.

Robertinho amesema, wanatakiwa kuwa makini wakiwa na mpira kwani itawasaidia kupunguza makosa ambayo yanaweza kuwagharimu.

Robertinho amesema, katika Ligi ya Mabingwa huwa hawaangalii ushindi mnono aliyeshinda bao moja na aliyeshinda tano wote wanapata pointi tatu hilo ndilo la umuhimu.

Pia Robertinho ameongeza kuwa, wanahitaji kupata alama tatu kesho ili kurejesha morali ya timu ingawa wanawaheshimu Vipers kutokana na ubora walio nao.

“Tunahitaji kuwa makini tukiwa na mpira, tumewasisitiza wachezaji kwenye kutumia nafasi tunazotengeneza, tunahitaji kupata alama tatu ugenini,” amesema Robertinho.

Kwa niaba ya wachezaji, mlinzi wa kati, Joash Onyango amesema, wamefika Uganda wakiwa wanajua mchezo utakuwa mgumu, Vipers ni timu bora lakini wamejipanga kuhakikisha wanapata alama tatu.

“Vipers ni timu nzuri, tunaiheshimu, lakini tumejipanga kikamilifu kuhakikisha tunashinda na kuchukua alama zote tatu ugenini,” amesema Onyango.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news