NA DIRAMAKINI
KOCHA Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera (Robertinho) ameonesha kufurahishwa na kiwango walichokionesha katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja.
Robertinho amesema, kilichomfurahisha ni jinsi walivyocheza kitimu hasa kipindi cha pili huku muunganiko wa wachezaji vijana na wazoefu ukiwa mzuri.

Ni kupitia mtanage wa nguvu ambao umepigwa Februari 25, 2023 katika Uwanja wa St.Mary's uliopo jijini Kampala nchini Uganda.
“Katika Ligi ya Mabingwa hasa hatua ya makundi ushindi ndilo jambo linalotakiwa, iwe moja, mbili au nne kinachoangaliwa ni pointi tatu.
“Tumecheza vizuri, tulikuwa na muunganiko mzuri mbinu yetu ilikuwa kuhakikisha tunapata ushindi, kipindi cha pili muunganiko wetu uliimarika, kasi iliongezeka iliyochangiwa na wachezaji vijana na wazoefu,” amesema Robertinho.
Robertinho pia amewasifu Vipers kwa mchezo mzuri na amekiri waliwapa upinzani mkubwa muda wote, lakini wao wamefanikiwa kupata ushindi.
“Haikuwa mechi rahisi, Vipers walikuwa washindani, wamecheza vizuri lakini tulizijua mbinu zao tukafanikiwa kuwathibiti,” amesema Robertinho.