Kwa nini NHC wameamua kuwa wehu wa maendeleo?

NA DIRAMAKINI

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu amesema, yeye na timu yake wameamua kuwa wehu (crazy) wa maendeleo ili kuhakikisha kasi inakuwa kubwa zaidi katika kutekeleza miradi mbalimbali ya shirika kwa ustawi bora wa shirika lenyewe,manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Shirika la Nyumba la Taifa lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na.45 ya mwaka 1962.NHC baadae liliunganishwa na iliyokuwa Msajili wa Majumba kwa Sheria Na. 2 ya mwaka 1990 ambayo ilirekebishwa mwaka 2005 ili kulifanya shirika lijiendeshe lenyewe kibiashara.

Malengo ya shirika kwa mujibu wa Mpango Mkakati wake (2015/16-2024/25) ni pamoja na kuwa msimamizi mahiri wa miliki, kuimarisha uwezo wa kiuendeshaji na udhibiti, kutumia kikamilifu rasilimali watu, kuwa kiongozi katika uendelezaji miliki, kuhuisha mikataba na mazingira ya kisheria na kujenga taswira ya shirika nchini.
Chini ya uongozi wa Mchechu, NHC limejiwekea maadili ya msingi sita ambayo ni weledi, ufanisi, uwazi, ubunifu, ushirikiano na uadilifu ili kuhakikisha wanapata matokeo chanya kwa haraka.

Mchechu ameyasema hayo Februari 17, 2023 jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini Hati ya Maelewano (MoU) baina ya Benki ya Absa Tanzania na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa lengo la benki hiyo kuwezesha wateja wake kupata mkopo ulioboreshwa kwa ajili ya manunuzi ya nyumba.

"Sisi kwa upande wetu kama NHC tulishasema tumeamua kuwa wehu wa maendeleo, miradi yetu mingi italenga sana soko la kati na chini kati, hiyo ndio itakuwa key driver, lakini soko la juu nao tutawapa vyao, lakini sisi tunakuwa tunaji-establish zaidi na kima cha kati na chini kati.

"Tuna miradi ya Samia Housing Scheme (SHS) ile ni miradi ambayo tunakwenda kuijenga Tanzania nzima, lakini focus kubwa iko Dar es Salaam na Dodoma na mikoani tutaenda, nyumba za Kawe tumezianza hatujatoka hata msingi asilimia 70 zimeshauzwa, lakini inatuambia kwamba bei tuliyoenda iko sahihi, tunajitahidi kwamba tusiwe na nyumba ya three bed room itakayozidi milioni 200, ndio lengo letu."
Mchechu amesema, shirika hilo limeamua kutekeleza miradi ambayo ina uwezo wa kutoa huduma zote za kijamii sehemu moja kama ilivyo huko nje, na ikikamilika Watanzania hawatakuwa na sababu ya kwenda Dubai kwa ajili ya kufanya manunuzi kwa sababu huduma zote zitapatikana sehemu moja kama itakavyokuwa Moroco Square.

"Tunahitaji nyumba tutakazo jenga ziwe katikati ya miji yetu yote ili Watanzania wasipate tabu ya usafiri, kwa hiyo sehemu ambayo tumejenga ni mbali ni kilomita tisa kutoka CBD leo ni Kawe hatuna mpango wa kwenda zaidi ya hapo na Kawe unasema asilimia 70 imeanza phase one imeshaisha na tutaenda kuanza phase two na tunaenda kumalizia ile miradi iliyokuwa imekwama.

"Lakini Kawe ile tunayojenga wakati tunaita leo iko kilomita tisa kutoka CBD actually sasa hivi nikikupa definition nzuri ya miaka mitano Kawe iko kilomita 0 kutoka the New Dar es Salaam CBD kwa sababu Kawe tunaenda tunai-transform kuwa CBD, tunatamani Kawe iwe ni mji ambao utakuwa relevant 50 years.

"Master Plan ya Kawe ambayo itabaki relevant maana yake ukinunua product yako una uhakika constantly over the 50 years ya pili uwe ni mji ambao uta-oparate for 24 hours for a day na kwa nini uwe hivyo? Dar es Salaam 60 percent ya GDP ina-exchange in Dar es Salaam."

"Kwa hoteli ambazo zinajengwa pale, entertainments zinazojengwa pale, office blocks zinazojengwa pale kwa sports arena ambayo Mheshimiwa Rais amezungumza na ame-commit na tumewapa kiwanja wanaenda kuanza ujenzi tunafikiri kwamba Kawe itakuwa 0 km to the CBD na huku Mjini nako tutakuwa O.2 km to the CBD wakati tunaendelea na Kawe tunakuja kushambulia Upanga.
"Tumeanza miradi ya ubia, lakini sehemu ambayo hatukutangaza ubia ni Upanga kwa sababu tunaanza kuanza kujenga ndani ya mwaka huu, tunataka mtu akitoka ofisini au kwake atembee kwa mguu kwenda lunch.

"Tunakwenda Dodoma kuimarisha middle shopping mall na what you see Morocco Square watakuwa na shops,hotels, malazi na tunataka kufanya uwe kisasa zaidi. Waziri wetu alituambia tuchape kazi na sisi tutachapa kazi kwa ufanisi tunachohitaji ni wehu wa maendeleo katika Serikali hii ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Hassan na ni kuchapa kazi tu,"amefafanua Mchechu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news