Kwa nini Vitamin A ina umuhimu kwa watoto?

NA DIRAMAKINI

WATAALAMU wa afya wanasisitiza kuwa,ili mtoto awe na afya bora anapaswa kupewa lishe bora. Hii ni lishe ambayo inatokana na makundi ya vyakula ambavyo vinatajwa kuwa na utajiri mkubwa wa vitamini na madini.

Vitamini A na Vitamin B humsaidia mtoto katika ukuaji na ukuaji na pia kumpa kiasi kinachohitajika cha kalsiamu na chuma.

Katika makala hii fupi kwa leo tuzungumzie Vitamin A. Kwa ujumla, kuna aina kuu mbili za vitamini A. Aina ya kwanza ni retinol ambayo haina rangi na inapatika tu katika vyakula vinavyotokana na wanyama, ndege na samaki.
Inaelezwa kuwa, vyanzo vikubwa vya vitamini A aina retinol ni maziwa ya mama, maziwa ya wanyama na maini.

Aina ya pili ya vitamini A ni carotenes ambayo ni ya rangi ya njano na inapatikana zaidi kutoka katika vyakula vyenye asili ya mimea.

Vyakula vyenye vitamini aina ya carotene ni pamoja na mapapai, matikiti, embe, mafuta mekundu ya mawese, samaki, karoti, viazi vitamu hasa vya rangi ya njano na mboga za majani zilizokolea ukijani.

Aidha,kwa ujumla vyakula vyenye vitamini A kwa wingi ni maziwa ya mama na zaidi yale ya kwanza (colostrum), ndege, samaki, maini za wanyama.

Wakati huo huo kiini cha yai, mafuta mekundi ya mawese, matunda yenye rangi ya njano kama papai, embe, mbogamboga za rangi ya njano kama karoti na matikiti, mboga za majani za kijani zaidi kama spinachi, kisamvu,mahindi ya njano, viazi vitamu vya rangi ya njano navyo vina utajiri mkubwa wa vitamin hizo.

Wataalamu wa afya wanasisitiza kuwa, jamii inaweza kuokoa gharama kubwa za matibabu ambazo zinachochewa na upungufu wa lishe kwa watoto kwa kuhakikisha kila mmoja anazingatia lishe kamili kwa ajili ya familia yake na watoto kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news