M-mama YASAIDIA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO LINDI

NA OR-TAMISEMI

MKOA wa Lindi umepiga hatua ya kupunguza vifo vya mama na mtoto kabla, wakati na baada ya kujifungua kutoka vifo 47 mwaka 2021 hadi vifo 32 mwaka 2022 ikiwa ni tofauti ya vifo 15 kwa mwaka.
Hayo yamebainishwa Februari 5,2023 na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Dkt. Kheri Kagya katika kikao kazi cha timu ya Usimamizi Shirikishi kutoka Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) na Timu ya Uendeshaji wa huduma za afya Mkoa wa Lindi.
Amesema,hatua hiyo imetokana na jitihada zinazofanywa na Serikali kwa kushirikiana na Vodafone, Touch Foundation pamoja na PathFinder katika kutokomeza vifo vya mama na mtoto nchini.

"Tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita kwa kushirikiana na Vodafone, Touch foundation na Pathfinder kupitia Mfumo wa usafirishaji kwa wajawazito na watoto wachanga (M-mama), tumeweza kupunguza vifo vya mama na mtoto na tunaendelea kuchapa kazi kuhakikisha tunatokomeza kabisa.
"Kupitia mfumo wa M-mama inapotokea changamoto ya kiafya kwa mama mjamzito au mtoto mchanga na anahitaji kupata rufaa kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine cha afya ili kupata huduma zaidi atapatiwa usafiri bure kwa kutumia magari ya kubebea wagonjwa au madereva jamii pasipo malipo yoyote kutoka kwa mhusika."

Naye Bi.Helena Mhagama ambaye ni muuguzi katika Mkoa wa Lindi amebanisha kuwa tangu kuanza kwa programu ya M-mama Julai 2022, wajawazito 965 na watoto wachanga 179 wamepata rufaa kupitia mfumo wa usafiri wa dharula (M-mama).

Kati ya rufaa zilizotumia magari ya wagonjwa ni 744 na ambazo zimetumia madereva jamii (community tax drivers) ni 392.

"Programu hii imesaidia kutambua maeneo ambayo yanahitaji uangalizi wa karibu wakati wa kutoa huduma ya mama na mtoto, kupata usafiri wa haraka zaidi pamoja na kutambua vituo gani vya afya vinatoa rufaa zaidi ili timu ya uendeshaji wa huduma za afya Mkoa iweze kufanyia kazi," amesema Mhagama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news