Mheshimiwa Abdulla atoa maagizo kwa bodi

NA DIRAMAKINI

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameipongeza Bodi ya Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na uongozi wake kwa kutekeleza kajukumu yao kwa mafanikio makubwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Bodi ya Wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi na uongozi wake waliofika kijitambulisha Ofisini kwake Vuga.

Mhe. Hemed ametoa pongezi hizo alipokutana na kufanya mazungumzo na Bodi hiyo Ofisini kwake Vuga Jijini Zanzibar.

Amesema ni muda mchache tokea kuanzishwa kwa wakala huo ambapo wameanza kutekeleza dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuwawezesha wananchi kupata mitaji na kutoa fursa za kukuza uchumi na kupunguza changamaoto zinazoikabili jamii.

Amesema, ni vyema wakala huo kuanzisha mifumo ya kieletroniki katika shughuli za uendeshaji ili kuweza kutoa huduma bora zaidi na gharama nafuu kwa wananchi.

Aidha, Mhe. Hemed ameridhishwa na utendaji kazi wa wakala kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na sekta binafsi na washirika wa maendeleo ndani na nje ya nchi katika utafutaji na upatikanaji wa rasilimali fedha.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Juma Amour Mohammed amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa baada ya kuchaguliwa kwa Bodi hiyo wameweza kutayarisha muundo wa taasisi pamoja na kuandaa mpango mkakati na kuratibu upatikanaji wa rasilimali fedha.

Aidha ameeleza kuwa Bodi inaendelea na mazungumzo na wadau mbali mbali wa Maendeleo kwa lengo la kukuza sekta ya Uwezeshaji nchini.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa wakala wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi Ndg. Juma Burhan amesema kuwa jumla ya wananchi 17,665 wamenufaika na fedha za uwezeshaji kati ya hao 8686 kutoka unguja wakiwemo wanaume 3311 na wanawake 5375 aidha kwa upande wa Pemba jumla ya wananchi 8979 wamenufaika wakiwemo wanaume 3425 na wanawake 5554.

Wakati wa mchana Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amejumuika na waumini wa Masjid JUMUIYA YA WAARABU RAHA LEO katika Ibada ya Sala ya Ijumaa na kuwataka waumini hao kudumisha Umoja na Ushirikiano katika jamii ili kudumisha upendo kwa Wazanzibari.

Mhe Hemed amewataka wafanya biashara kuwa na Imani na uadilifu katika biashara zao kama ilivyoelekezwa katika kitabu kitukufu cha qur-an juu ya ufanyaji wa biashara na faida zake.

Amesema kufanya hivyo kutapelekea wananchi kuwa na Imani na wafanya biashara pamoja na Serikali yao amabayo imetoa muungozo juu ya ufanyaji wa biashara nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news