Februari 14, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ambapo amemuhamishia, Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii huku Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii akihamishiwa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Rais Dkt.Samia pia amemuhamishia Dkt.Hassan Abbas Said, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii akichukua nafasi ya Profesa Eliamani M. Sedoyeka.
Uongozi wa DIRAMAKINI unawapongeza kwa kuendelea kuaminiwa na Rais Dkt.Samia katika kumsaidia kutekeleza majukumu muhimu kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii.
DIRAMAKINI inaamini kwa ubunifu na mikakati yenu, Sekta ya Utalii Tanzania inakwenda kuvushwa hatua nyingine...HONGERENI SANA MHESHIMIWA MCHENGERWA NA DKT.ABBAS.