NA ALBANO MIDELO
MSITU wa Hifadhi wa Taifa wa Mazingira Asilia Mwambesi uliopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma ulianzishwa mwaka 1956 na ulipandishwa hadhi kuwa msitu wa Taifa katika kipindi cha mwaka 2017/2018.
Anawataja wanyama waliopo katika msitu huo ambao upo kandokando mwa Mto Ruvuma kuwa ni simba, tembo, chui,kuro,jamii za nyani,jamii za swala,nyati na wanyama wengine.
Kwa mujibu wa Mwangama, ndege huyo ana tabia ya kuzamia samaki kutoka majini na kwamba ndege hao wanapenda kuishi kwenye maporomoko ya Mto Ruvuma yanayoitwa sunda ambayo yapo ndani ya hifadhi hiyo.

Kwa mujibu wa Mwangama, ndege huyu huogolea kwa kufuata mdondoko wa mawimbi ya maji kwenye maporomoko hayo akitatafuta mawindo yake ya samaki ambacho ndicho chakula chake pekee.
Licha ya ndege huyo Mwangama anayataja maporomoko ya Sunda kuwa ni miongoni mwa vivutio vya utalii katika hifadhi ya Mwambesi na kwamba maporomoko hayo yalitumika wakati wa vita ya Majimaji kati ya mwaka 1905 hadi 1907 ili kujificha kwenye mapango kwa juu.
Anasema, mto huo ndio uliokuwa ukitumika kwenye vita vya Majimaji ambapo watu wa makabila au ukanda wa Kusini hususani Wangoni walitumia maji yake katika kuzimia silaha za moto chini ya uongozi wa Kinjeketile Ngwale.
Kulingana na Mwangama, eneo hilo pia linaaminika Wajerumani walitumia kama njia kubwa wakitokea Msumbiji katika biashara ya meno ya Tembo na kwamba Waarabu walipita pembezoni mwa mto huo kuwapitishia watumwa.
Hata hivyo anasema awali kabla ya serikali kuamua msitu huo kuwa Msitu wa hifadhi,kulikuwa na vitalu vya uwindaji wa kitalii ambapo ndani ya msitu kulikuwa na kambi ya wawindaji iliyoitwa Big Game iliyoendeshwa na Kampuni ya uwindaji iliyoitwa Tandara Hunting Safaris.
Kulingana na Meneja huyo,msitu huo una ukubwa wa zaidi ya hekta 112,000 na kwamba mtalii akiwa katika msitu wa Mwambesi anaweza kufanya utalii wa kuteleza kwenye mitumbwi katika mto Ruvuma.
Deborah Mwakanosya ni Meneja wa Msitu anasema, Mwambesi ni msitu wa asili wa pili kwa ukubwa kwa Tanzania ukiongozwa na msitu wa Kilombero mkoani Morogoro.

Mwambesi ni moja kati ya Misitu mikubwa ya Hifadhi za Mazingira Asilia tulionayo wenye utajiri mwingi wa flora na fauna zakutosha.Msitu wa Mwambesi unahifadhiwa kisheria chini ya uangalizi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kwa kushirikina na Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU) Kanda ya Kusini.