Prof.Muhongo ageukia ujenzi wa maabara za sayansi shuleni

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo ameendesha harambee kwa ajili ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi za Shule ya Sekondari Seka katika Kata ya Nyamrandirira yenye vijiji vitano.
Seka Sekondari ni sekondari ya pili ya Kata ya Nyamrandirira yenye vijiji vitano. Sekondari hii iliyojengwa katika Kijiji cha Seka, Musoma Vijijini ilifunguliwa Julai 5,2021.

Aidha,sekondari ina jumla ya wanafunzi 344 (vidato vya I, II & III) na walimu tisa, mmoja akiwa ni wa kujitolea. Mapungufu makubwa na muhimu ni ukosefu wa maabara tatu za masomo ya sayansi ya Fizikia, Kemia na Baiolojia. Pia kuna uhitaji wa Maktaba, choo kingine chenye matundu saba na jengo la utawala.
Harambee hiyo imefanyika Februari 2, 2023 ambapo Mbunge wa jimbo hilo, Mheshimiwa Prof. Muhongo amechangia saruji mifuko 150, vitabu vya Maktaba boksi saba,mahindi magunia manne ya chakula cha wanafunzi. Huku viongozi mbalimbali wa kata hiyo wakiongozwa na Diwani wao Mheshimiwa Mwalimu Nyeoje wamechangia saruji mifuko 12 na fedha taslimu shilingi 100,000.

Aidha, kutokana na msukumo wa dhati wa wanavijiji wameamua kwamba maabara hizo zikamilike ifikapo Juni 30,2023. Wanavijiji watachangia nguvu kazi na shilingi 15,000 kila kaya, sambamba na vifaa vya ujenzi vilivyosalia kwenye ujenzi wa kutumia fedha za Serikali, vitumike mara moja, ikiwemo saruji mifuko 60.
Aidha, taarifa ilitolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini imesema, "Ombi maalumu la Uongozi wa shule ya Seka Sekondari isaidiwe kupata,kompyuta, printer na photocopying machine- wanakijiji na Mbunge wao wa Jimbo, watachanga kwa pamoja na kuvinunua ifikapo Aprili 30,2023," imeeleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa.

"Michango ya awali ya ujenzi wa Seka Sekondari ilianza kujengwa kwa nguvu za wanavijiji, Mbunge wa Jimbo , wazaliwa wa Kata ya Nyamrandirira na baadae serikali imetoa michango mikubwa. ambapo wanavijiji wamejitolea nguvu kazi kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji. Kijiji cha Seka kilijenga na kuezeka vyumba vitatu vya madarasa na kununua samani za ofisi za walimu.
"Kijiji cha Kasoma kilijenga na kuezeka vyumba viwili vya madarasa. Vijiji vya Mikuyu na Kaboni vilijenga na kuezeka maboma mawili ya madarasa.

"Kijiji cha Chumwi kilichangia ujenzi wa boma moja la darasa na ujenzi wa choo cha walimu. Wazazi wanachangia malipo ya posho za walimu wa kujitolea.

Ambapo Serikali imechangia, kwa nyakati tofauti shilingi milioni 25 + 80 + 60. Vifaa vya Maabara na shilingi 891,436,- kila mwezi (uendeshaji) kuanzia Oktoba 2022," imesema taarifa hiyo na kuongeza kuwa,
"Wanavijiji wa Kata ya Nyamrandirira na viongozi wao mbalimbali wanatoa shukrani za kipekee kwa Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa mchango mkubwa, wa ujenzi wa sekondari yao, unaotolewa wa Serikali anayoingoza."
"Mbunge wa Jimbo Michango yake ya awali, kwa nyakati tofauti, ni Saruji Mifuko 200, Mabati 120. Mfuko wa Jimbo umechangia Saruji Mifuko 330, Mabati 137, Nondo 17, na Wazaliwa wa Kata ya Nyamrandirira wamechangia jumla ya shilingi 2,840,000. Huku Halmashauri yetu hadi sasa mchango wake ni saruji mifuko 30 tu. Mgodi wa Seka Mchango wa Mgodi huu (MMG) wa dhahabu ni mdogo na hauridhishi,"imeongeza taarifa hiyo.
Picha juu zinaonesha matukio mbalimbali ya harambee iliyofanyika Februari 2, 2023 Seka Sekondari iliyopo Musoma Vijijini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news