NA DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Februari 8, 2023 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said, Mheshimiwa Rais amemteua Dkt.Mohamed Hafidh Khalfan kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani Halali wa Biashara Zanzibar.
Aidha, kabla ya uteuzi huo, Dkt.Mohamed alikuwa ni Mjumbe wa Tume ya Ushindani Halali wa Biashara Zanzibar na uteuzi wake umeanza rasmi Februari 8, 2023.
Aidha, kabla ya uteuzi huo, Dkt.Mohamed alikuwa ni Mjumbe wa Tume ya Ushindani Halali wa Biashara Zanzibar na uteuzi wake umeanza rasmi Februari 8, 2023.