
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mwakilishi na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Kanda ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika, Bw.Marcel Akpovo alipofika Ikulu jijini Zanzibar na ujumbe wake.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Kanda ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika, Bw.Marcel Akpovo, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.