NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Said Ally Mohamed kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 27, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunusu ambapo uteuzi huu umeanza Februari 23, 2023.