NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 14, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus ambapo uteuzi huu umeanza Februari 9, 2023.
Pia Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Marwa Waitara kwa kipindi kingine kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi Tanzania (TANAPA).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Marwa Waitara umeanza Februari 13, 2023.