NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Mhandisi Yahya Ismail Samamba kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini.
Kabla ya uteuzi huu Mhandisi Yahya Ismail Samamba alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,Zuhura Yunus uteuzi huo umeanza tarehe 27 Februari, 2023.