NA DIRAMAKINI
MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kununua kila bao litakalofungwa na Simba SC na Young Africans katika michuano ya CAF inaendelea.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Msigwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo amesema shilingi milioni tano kwa kila goli lililofungwa na vilabu hivyo vya Dar es Salaam itatolewa hadi mwisho wa mashindano ya CAF.
Simba SC wako Kundi C la Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa na vinara Raja Casablanca, Horoya na Vipers huku Young Africans ambao wanawakilisha kwa upande wa Michuano ya Shirikisho CAF ipo na TP Mazembe, US Monastir na De Bamako.
Mwishoni mwa wiki, Simba ilifungwa mabao 3-0 na Raja Casablanca ya Tunisia jijini Dar es Salaam na kukosa nafasi ya kuweka mfukoni kiasi cha fedha kilichoahidiwa na Rais Dkt.Samia.
Aidha, wapinzani wao wa jadi, Young Africans waliibuka wanufaika wa ahadi ya Rais Dkt.Samia baada ya kuichapa TP Mazembe ya DRC mabao 3-1 jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili jioni na kuondoka na jumla ya shilingi milioni 15.