NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Kenya,Mheshimiwa William Samoei arap Ruto amesema, Serikali imejitolea kutoa fedha kwa wakati kwa serikali za kaunti.

Picha na Ikulu.
Mheshimiwa Rais Ruto amesema, utekelezaji huo utasaidia kuharakisha ugatuzi na kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi.
Rais amebainisha kuwa, vitengo vya utawala vilivyogatuliwa ndivyo kitovu cha maendeleo ya Kenya. Pia ameahidi kufanya kazi kwa karibu na kaunti na "kuongeza ushirikiano wetu", hasa katika kilimo, usalama, afya na makazi.

Naibu Rais Rigathi Gachagua, Mwenyekiti wa Baraza la Magavana Ann Waiguru, Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula, Spika wa Seneti Amason Kingi, Mwanasheria Mkuu Justin Muturi, Magavana, walikuwa ni miongoni mwa wageni wengine waliohudhuria.

“Inachelewesha utekelezaji, inawanyima Wakenya haki yao ya kupata huduma, lazima tuwe na nia moja."

Bw. Gachagua alisema ni lengo la Serikali kuhakikisha ugatuzi unafaulu.Alibainisha kuwa, kupitia ushirikiano mzuri na wenye kujenga na Serikali ya Kitaifa, kaunti zina uwezo wa kuibadilisha Kenya.