SHIRIKINI MIKUTANO YA MAENDELEO

NA ADELADIUS MAKWEGA

BIBI Maendeleo wa Kata ya Chamwino Ikulu jijini Dodoma,Juliana Mtolela amesema kuwa jamii ya eneo hilo haishiriki mikutano ya maendeleo kila inapoitishwa, lakini imeendelea kwenda katika nyumba ya ibada kusali, akiomba pia wakazi wa eneo hilo washiriki mikutano ya kimaendeleo maana nayo ina manufaa makubwa katika kipindi cha sasa na kutokushiriki kwa wananchi kunasababisha maafisa maendeleo sasa kuzunguka katika nyumba hizo za ibada kueleza mambo kadhaa ya maendeleo.
Hayo yamebainishwa katika matangazo ya misa ya dominka ya tano ya mwaka A wa liturijia , katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata, Parokia ya Chamwino Ikulu, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Februari 5, 2023.

“Kwa sasa kumekuwa na kuongezeka kwa vitendo vibaya hasa makuzi na udhalilishaji wa watoto ambao ni ukatli wa kijinsia, nje utaliona eneo letu ni salama lakini siyo salama kwa matukio hayo.”

Alisema kuwa, yeye yu kanisa kuhamasisha wazazi na walezi wawe wa kwanza kutunza watoto wao, walimu kule shuleni jukumu lao ni kuwafundisha na kule, lakini malezi yanaanzia nyumbani.

Kama baba au mama hatachukua hatua ya kutunza mtoto wake hadhani kama kuna mtu mwngine atatimiza wajibu huo mkubwa.

“Watoto wanafanyiwa vitendo vya unajisi na ulawiti, si vizuri, kwa hiyo tuchukue hatua, nashukuru sana Baba Padri katika nyumba za ibada watu bado wanafika, tunawaombeni pia mjitokeze katika mikutano ya kijamiii,nayo ni kwa ajili yenu, tunawaambia leo linamkuta mtoto wa mwenzako lakini kesho ni la mtoto wako.”

Awali katika mahubiri ya misa hiyo Padri Paul Mapalala alitilia maanani kwa kila Mkristo kuwajibika kuyatekeleza yale aliyoyaapa katika Sakramenti zote za Kanisa.

Jipige picha kuona je jamii inayokuzunguka inakutazamaje wewe kama Mkristo? Inavutiwa na maisha yako ? Au umekuwa muharibifu? Alihoji Paroko huyo.

“Masomo ya leo yanatukumbusha wajibu wetu kama Wakristo, tangu tumebatizwa tumewavuta wangapi kwa Kristo? Au tumekuwa vikwazo katika familia, jumuiya na jamiii zetu.”

Misa hiyo ya kwanza iliyoanza saa 12. 00 ya Asubuhi iliambatana maombi kadhaa mojawapo lilikuwa hili,“Kwa nguvu ya Roho Mtakatifu utuhamasishe tujue imani yetu barabara na kuitetea bila hofu.”

Wakati misa inafikia ukingoni, msomaji wa matangazo alimualika Padri John Greyson kutoka Shirika la Damu Takatifu ya Yesu anayefanya utume Miuji katika nyumba ya malezi pia anahudumia Kigango cha Buigiri kilicho chini ya Parokia ya Chamwino Padri aliwaomba waamini kanisani hapo kujiunga shirika lao ambao kila mlei aliyebatiza, kupata Komuniyo na Kipaimaar anaweza kujiunga nao.

Mpaka misa hiyo inamalizika hali ya hewa ya eneo la Chamwino Ikulu kwa juma nzima kidogo imebadilka ambapo jua kali limepunga, huku mvua kiasi imeipoza ardhi ya eneo nayo mahindi na mazao mengine yakiendelea kumea vizuri

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news